Sunday, January 29, 2012

JMAW - Watoto Uwaleavyo Nao Ndivyo Wakuavyo

Ewe Mama Mjasiri, Sikia Niyasemayo
Si Maneno ya Adhiri, Ila Kuwa Egemeo
Siwa ache chachari, Watoto Uwaleyao
Watoto Uwaleavyo, Navyo Ndivyo Wakuavyo

Mfundishe ya misemo, Na Methali 'nazofaa
Usikuwe na muwamo, zitazompa dondoa
Usimpomfunza thumo, Dunia Tamfunzua
Watoto Uwaleavyo, Navyo Ndivyo Wakuavyo

Simzoeshe anasa, siku atakapokosa
Atageuka muwasa, nawe ndiwe wa makosa
Akifungwa kwa makosa, we msababisha kisa
Watoto Uwaleavyo, Navyo Ndivyo Wakuavyo

Sipokatazwa kuiba, 'tendelea vyo daima
Alianza kule nyumba, halafu sasa lawama
'Ngalikatazwa kuiba, ngalikuwa mzima
Watoto Uwaleavyo, Navyo Ndivyo Wakuavyo

Sipofunzwa egemeo, Kweli utasikitika
Kwa misemo ile yao, waswahili huitika
Maji yaliyomwagwayo, Hayawezi kuzoleka
Asofunza na mamaye, hufunzwa na ulimwengu

No comments:

Post a Comment