Friday, August 3, 2012

JMAW - Huu ukulima gani, usiwo umadhubuti?

Wizara ya Ukulima, Watu  twawalilieni
Mbegu zetu zimenyima, kweli sasa kuna nini?
Afisa Afisi Nzima, Saa zote ni kitini
Tembeeni Mashambani, Kenya tupate uzima

Kila siku shambani, Asubuhi na mapema
Mwalima fikirini, Mbona mazao si mema?
Twaomba saidieni, Afisa wa ukulima
Tembeeni mashambani, Kenya tupate uzima

Asubuhi kavaa suti, ati yuenda kazini
Kazi yake ni kuketi, kwani yuandika nini?
Kisha kasoma gazeti, angoja kwenda nyumbani
Huu ukulima gani, usiwo umadhubuti

Mbolea tumenunua, urea na kadhalika
Hatujapata kujua, mbolea navyotumika
Ni heri kama mwajua, kwanini twataabika
Kaeni ndani madukani, taabu tufananua

Raisi katoa wito, Rudini kwenu shambani
Kwani ninyi watoto, 'sojua bora ninini?
Hebu fateni wito, shambani ndipo kazini
Kulima siyo kuzini, Na shamba si penye moto

Huu ukulima gani, usiwo umadhubuti?

No comments:

Post a Comment